Haya tena nimekusogezea vionjo vya hadithi za jarida la Sani juu na jarida la Bongo hizi mbili chini lililokuja baadaye miaka ya 90. Juu kabisa ni toleo la kufunga mwaka 86-87 nakumbuka nilikuwa bado mdogo nadhani nilikiuwa darasa la 2 kipindi hicho. Majarida ya mwisho wa miaka ya 80 kuelekea 90 ndo nilianza kuyafuatilia sana na yalikuwa yanatoka kila mwezi na hadithi za kusisimua sana akina chepe, kipepe, sokomoko, ndumilkuwili, lodilofa, madenge, kifimbo cheza, dokta pimbi, nakumbuka pia kulikuwa na kurasa kadhaa za vichekesho ilikuwa inaitwa cheka unenepe, ikifuatiwa na hadithi za wimbi la Kitintale unakutana na akina Obi, Linda, zumo, bosi mayuyu liyekuwa anaishi kisiwani aliyekuwa anafanya biashara za madawa ya kulevya na magenge yake ya unyang'anyi, Ole aliyekuwa mtesaji wa huyo mdosi na mabaunsa wenzake. Riwaya za akina Eddy Genzel mauaji ya hayawani, kizaizai na nyinginezo zilizokuwemo kwnye hilo jarida. Hizi mbiliza chini mchoraji ni John Kaduma. Pia nakumbuka huyu