Jarida la Sani+Bongo



Haya tena nimekusogezea vionjo vya hadithi za jarida la Sani juu na jarida la Bongo hizi mbili chini lililokuja baadaye miaka ya 90. Juu kabisa ni toleo la kufunga mwaka 86-87 nakumbuka nilikuwa bado mdogo nadhani nilikiuwa darasa la 2 kipindi hicho. Majarida ya mwisho wa miaka ya 80 kuelekea 90 ndo nilianza kuyafuatilia sana na yalikuwa yanatoka kila mwezi na hadithi za kusisimua sana akina chepe, kipepe, sokomoko, ndumilkuwili, lodilofa, madenge, kifimbo cheza, dokta pimbi, nakumbuka pia kulikuwa na kurasa kadhaa za vichekesho ilikuwa inaitwa cheka unenepe, ikifuatiwa na hadithi za wimbi la Kitintale unakutana na akina Obi, Linda, zumo, bosi mayuyu liyekuwa anaishi kisiwani aliyekuwa anafanya biashara za madawa ya kulevya na magenge yake ya unyang'anyi, Ole aliyekuwa mtesaji wa huyo mdosi na mabaunsa wenzake. Riwaya za akina Eddy Genzel mauaji ya hayawani, kizaizai na nyinginezo zilizokuwemo kwnye hilo jarida. Hizi mbiliza chini mchoraji ni John Kaduma. Pia nakumbuka huyu jamaa alikuwa na vijitabu vyake vya hadithi za kichawi vilivyoitwa Panga la Shaba. Jamaa alikuwa mkali sana wa kuchora ni hadithi za michoro kuanzia mwanzo mpaka mwisho. Huyu Panga la Shaba alikuwa anaishi kijijini na alikuwa ni mganga wa kienyeji anayetumia uchawi kuloga na kuwapa watu nguvu za kichawi. Usafiri wake ulikuwa ungo na alikuwa anakula panya na ugali mkubwa sana. Ukiingia kwake ni hirizi na matunguri na vifaa vya waganga kila mahali. Jamaa alikuwa na fikra za ajabu sana sikumbuki mbunifu wa hizi hadithi kama alikuwa yeye mwenyewe au nani hasa?  Matajiri walikuwa wanatoka mijini kwenda kwake kijijini kupatiwa bahati za kuwa matajiri na kupoendwa na mabinti wakali sasa hilo balaa lake aliokuwa nasababisha mambo yasipokwenda vizuri na alikuwa analeta mitafaruku na maofisa wa usalama kutokana na uchawi wake. Sijui hivi vijitabu viliishia wapi lakini nachokumbuka ni ile michoro yake niilipenda sana. Kutokana na umakini na usanifu mzuri aliokuwa nao kwenye kuwachora akina Panga la shaba na wafanyabishara wenye pesa na wadada wazuri. Michoro yake ilikuwa inaongea naweza kusema hivyo. RIP gwiji John Kaduma aka John Black.

Comments

Popular posts from this blog

Kadi ya mchango wa harusi

Kadi mchango wa harusi