Enzi za Sani
Dah za jarida la sani-burudisho la wasomaji. Nilipenda sana kulisoma hili jarida miaka ile ya 1985-1996. Sikuwahi kukosa toleo hata moja na visa vya akina Pimbi, Ndumilakuwili, kipepe, sokomoko, Lodi lofa na hadithi za akina Obi na Linda. Nilimhusudu mchoraji gwiji marehemu John Kaduma akishirikiana na Ted Marealle na akina Ndunguru alienza kuchora miaka ya mwanzoni ya 80 na baadaye kuwaachia waliofuata yaani akina Kaduma na wengineo. Yeye ndo mbunifu wa hilo gazeti na hao characters niliowataja na mtunzi wa riwaya ndefu Bawji naye marehemu. Nimewawekea baadhi ya machapisho niliyoyapata mtandaoni, Hizo hapo chini ni hemu ya hadithi ya Obi na Linda ktk kisa cha huyo mfanyabishara wa madawa ya kulevya Mayuku. Obi akiwa porini akipambana na maajenti wa Mayuku-visa vya uharamia na madawa ya kulevya nilivipenda sana kuvifuatilia. Sijui haya magazeti yanapatika wapi kwa sasa niwe na library yangu. K wa vijana wa sasa onjeni uhondo huo wa miaka ya nyuma tulipokuwa tunakua na kusoma haya magazeti na mengineyo ya Bongo na tabasamu. Yalikuja kupotea miaka ya 2000-2001 likabaki sani tu ambalo lilianza kutoka kama gazeti ambalo liliingizwa habari za udaku na kupoteza ule mvuto na hadithi na visa vya miaka hiyo.
Comments
Post a Comment